ELIMU, TEKNOLOJIA NA UONGOZI VYATAJWA KUWA SILAHA YA MAGEUZI
Na Mwandishi wetu,
WAKATI Dunia ikielekea zaidi kwenye uchumi na huduma za kidijitali, wanawake wa Jeshi la Magereza Tanzania wametakiwa kutokaa nyuma, bali kuongeza elimu, ujuzi na uwezo wa kutumia teknolojia ili kushika nafasi zaidi za uongozi na kitaaluma.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mtandao wa Wanawake Jeshi la Magereza Tanzania (TPSWNet) 2026 jijini Dodoma.
Mahundi amesema ushindani wa sasa unahitaji watumishi wanaojifunza kwa kuendelea na kutumia teknolojia kuboresha huduma.
Kwa upande wake, CP Nicodemus Menyiansumba Tenga, Kamishna wa Divisheni ya Sheria na Uendeshaji wa Magereza, amesema mafanikio ya wanawake waliopo kwenye nafasi mbalimbali ni mfano wa kuhamasisha wengine.
CP Amina Jumanne Kavirondo, Kamishna wa Huduma za Urekebishaji Jeshi la Magereza, amesema TPSWNet inaendelea kujenga uwezo, kukuza usawa wa kijinsia na kuboresha mazingira ya kazi kwa wanawake.
Mkutano huo unaofanyika Septemba 7 hadi 9, 2026, unajadili uongozi, uwezeshaji wa kiuchumi, afya, maadili, matumizi sahihi ya mitandao na urekebishaji wa wafungwa.
Leave a Comment